Andika. Chapisha.
Pata malipo.
Geuza hadithi zako kuwa kipato. Chapisha simulizi zako kwenye Kurasa, wasomaji wazisome, na upate mgao wa mapato — hela moja kwa moja kwenye simu yako.
Mgao wako
60%
Unabaki na 60% ya kila malipo yanayotokana na hadithi zako. Kurasa inabaki na 40% kugharamia mfumo wa malipo, tovuti, na kukuza hadithi zako kwa wasomaji wapya.
Jinsi inavyofanya kazi
Jiunge kwa mualiko
Programu ni ya mualiko. Ukipata kiungo cha kujiunga kutoka kwa Kurasa, unafungua akaunti yako ya mwandishi kwa dakika chache.
Andika na kuchapisha
Andika hadithi zako moja kwa moja kwenye Kurasa — weka picha, gawa kwa kurasa (sehemu), kisha chapisha. Unatumia jina lako la kalamu.
Wasomaji wanasoma na kulipa
Wasomaji hulipa kusoma hadithi zako. Kila malipo yanayotokana na hadithi yako, unapata mgao wako moja kwa moja.
Toa fedha zako
Salio lako linaonekana kwenye dashibodi yako. Ukifikia TZS 10,000, unaomba kutoa fedha kwa M-Pesa, Tigo Pesa au Airtel Money.
Mfano wa mapato
Tuseme una hadithi ya kurasa 10, na wasomaji 100 wanaisoma yote. Kila ukurasa unagharimu 100 credits (TZS 100) kwa msomaji.
- Wasomaji wanalipa jumla
- TZS 100,000
- Mgao wa Kurasa (40%)
- −TZS 40,000
- Unapata wewe (60%)
- TZS 60,000
Hiyo ni takribani TZS 60 kwa kila ukurasa unaosomwa. Kadiri hadithi zako zinavyosomwa zaidi, ndivyo mapato yako yanavyoongezeka — bila kikomo.
Kadiri wasomaji wanavyoongezeka
Tuseme kila msomaji anayelipa anasoma takribani kurasa 8 za hadithi yako — hapo unapata 480 TZS kwa kila mmoja (60% ya walichotumia).
| Wageni | 10% wanaolipa | 15% wanaolipa | 20% wanaolipa |
|---|---|---|---|
| 1k | TZS 48,000100 watu | TZS 72,000150 watu | TZS 96,000200 watu |
| 10k | TZS 480,0001,000 watu | TZS 720,0001,500 watu | TZS 960,0002,000 watu |
| 50k | TZS 2,400,0005,000 watu | TZS 3,600,0007,500 watu | TZS 4,800,00010,000 watu |
| 100k | TZS 4,800,00010,000 watu | TZS 7,200,00015,000 watu | TZS 9,600,00020,000 watu |
Mfano wa makadirio tu — mapato halisi hutegemea idadi ya wanaolipa na wanavyoendelea kulipa.
Ukurasa wako binafsi
Unapata ukurasa wako (kurasa.co.tz/author/jina-lako) unaoonyesha hadithi zako zote mahali pamoja.
Toa fedha wakati wowote
Hakuna kusubiri mwisho wa mwezi. Ukifikia TZS 10,000, omba na upokee kwenye simu yako.
Mapato yasiyo na kikomo
Hadithi nzuri huendelea kusomwa kwa miezi. Unaendelea kupata kila inaposomwa.
Una nia ya kuandika nasi?
Jaza fomu ya maombi na uambatanishe viungo vya kazi zako ulizochapisha mitandaoni. Tukikagua na kuridhika, utakubaliwa kuanza kuchapisha hadithi zako hapa.
Omba kuwa mwandishiUna swali? Tembelea Wasiliana Nasi.
Asilimia na viwango vinaweza kubadilika. Waandishi hujulishwa kabla ya mabadiliko yoyote.